Karagwe FM
Karagwe FM
8 March 2025, 6:02 pm

Kutokana na ongezeko la malalamiko ya wananchi wanaotumia nishati ya gesi mkoani Kagera kuishiwa gesi ndani ya muda mfupi watumiaji wote wa gesi wameaswa kuwa makini na mitungi wanayonunua kwa kuhakiki uzito kabla ya kufanya manunuzi
Theophilida Felician.
Watumiaji wa nishati ya gesi mkoani Kagera wameshauriwa kupima mitungi hiyo ya gesi kabla ya kufanya ununuzi ili kujiridhisha na kiwango cha ujazo jambo litakalosaidia kuepusha changamoto ya kuuziwa mitungi yenye upungufu wa ujazo.
Ameyasema hayo afisa huduma kwa wateja wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji EWURA CCC wakati akizungumza na Radio Karagwe ofisini kwake Manispaa ya Bukoba.
Afisa huyo amesema baadhi ya wananchi hulalamikia changamoto ya kununua gesi na kuisha matumizi kwa muda mfupi jambo linaweza changiwa na sababu mbalimbali ikiwepo ya upungufu wa ujazo hivyo ni vyema wakazingatia suala la upimaji kabla ya ununuzi ili kuepusha hali hiyo.
Hata hivyo amewasisitiza watumiaji wa gesi kuitumia kwa tahadhari kubwa ya kuzingatia maelekezo wanayopewa ili kuepukana na madhara ya kulipuka akitolea mfano kwamba unakuta mtu anapika kwenye mtungi pembeni kaweka jiko la mkaa linawaka hali ambayo ni hatarishi.