Karagwe FM
Karagwe FM
1 March 2025, 9:42 am

Ofisi za uthibiti ubora wa elimu katika halmashauri za wilaya mkoani Kagera zimeendelea na ufuatiliaji wa miradi ya elimu na kuishukuru serikali kwa jinsi inavyoendelea kusajili na kusimamia shule za msingi na sekondari
Na Ezra Lugakila
Afisa uthibiti ubora wa elimu wilayani Kyerwa mkoani Kagera Mwalimu Damian Barabona ameishukuru serikali kwa kuendelea kuipa fedha idara ya uthibiti ubora za usimamizi na ufuatiliaji ili kufikia mafanikio yaliyopo kwa kipindi cha kuanzia 2020 hadi 2025
Akizungumza na Radio Karagwe wakati akieleza mambo mbalimbali kuhusu idara hiyo afisa uthibiti ubora wa elimu wilayani Kyerwa Mwalimu Barabona serikali wilayani Kyerwa imesajili shule nyingi za sekondari sambamba na kuboresha miundombinu kwa shule za zamani
Pamoja na ufanisi katika miundombinu ya shule Bw. Barabona amesema kuwa idara ya uthibiti ubora wa shule imeendelea kuhamasisha vipindi vya elimu ya dini shuleni ili kuwaandaa vijana na jamii kwa ujumla wenye maadili na uzalendo