Karagwe FM
Karagwe FM
24 February 2025, 7:04 pm

Kikundi cha mtandao wa WhatsApp kijulikanacho kama Buhaya Tegeka wilayani Missenyi mkoani Kagera kimetoa mfano wa kunufaisha jamii kuliko kujinufaisha chenyewe kwa kuchangia vitu kadhaa vya mahitaji ya watoto
Na,
Respicius John, Missenyi-Kagera
Kikundi cha mtandao wa Whatsapp cha Buhaya tegeka kimeadhimisha miaka minne ya kuanzishwa kwake kwa kutoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja na nusu kwa watoto wanaoishi katika mazingira Magumu wilayani Missenyi
Hafla fupi ya kukabidhi zawadi hizo imefanyika katika kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Magharibi mtaa wa Kashozi wilayani Missenyi kwa kugawa zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 zimetolewa kwa watoto wanaolelewa na kituo cha mtoto na kijana ELCT Kashozi
Makamu mwenyekiti wa kikundi hicho Moses Ignatio amesema kuwa kikundi cha Buhaya Tegeka wameamua kufanya matendo ya huruma wakati wakiadhimisha miaka mine tangu kianzishwe mtandaoni ambapo pia mmoja wa wanakikundi amesema kuwa tendo hilo ni kurudisha fadhila kwa jamii inayowazunguka

Mwenyekiti wa uwakili kanisani hapo Mwalimu Julius Mulokozi amewashukuru watu wa kikundi hicho na kutoa wito kwa vikundi vingine kuiga mfano wa kikundi hicho
