Karagwe FM

CCM Kagera yaonya wanaounda makundi kabla ya uteuzi wa wagombea

5 February 2025, 11:48 am

katibu wa itikadi uenezi na mafunzo wa chama cha mapinduzi mkoa wa Kagera Hamimu Mahamud,wakati akihutubia wananchi waliohudhuria sherehe ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi iliyofanyika kimkoa wilayani Missenyi.picha na Respicius John

Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Kagera kimeahidi kuleta wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani katika mwaka wa uchaguzi 2025 watakaotokana na wananchi na waliopita katika utaratibu

Na Respicius John, Missenyi-Kagera

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Kagera wametakiwa kuwa watulivu katika kipindi hiki hadi mchakato wa kupata wagombea wa nafasi ya ubunge na udiwani kwa tiketi ya chama hicho utakapokamilika.

Wito huo umetolewa na katibu wa itikadi uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Kagera Hamimu Mahamud, wakati akihutubia wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 48 ya chama hicho zilizofanyika kimkoa katika kata ya Kitobo wilayani Missenyi mkoani Kagera

Pia amewahakikishia wana CCM kuwa chama kitapitisha wagombea wenye sifa watakaokiwezesha kupata ushindi wakati wa uchaguzi mkuu 2025

Sauti ya katibu wa itikadi uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Kagera Hamimu Mahamud
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Projestus Tegamaisho. Picha na Respicius John

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misenyi Projestus Tegamaisho amesema kuwa lengo la halmashauri anayoiongoza ni kuhakikisha anaondoa michango ambayo ni kero kwa wananchi

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Projestus Tegamaisho
Mbunge wa jimbo la Nkenge Florent Kyombo. Picha na Respicius John

Mbunge wa jimbo la Nkenge Florent Kyombo kwa upande wake amesema katika kuendelea kuunga mkono juhudi za Dkt Samia Suluhu Hassan atawanunulia sale za chama cha mapinduzi viongozi wa ccm

Sauti ya mbunge wa jimbo la Nkenge Florent Kyombo