Karagwe FM
Karagwe FM
4 February 2025, 10:24 am

Kumekuwa na malalamiko juu ya upatikanaji wa haki mahakamani kwa makundi mbalimbali wakiwemo wajane wanaolalamikia kunyanyasika pindi wenza wao wanapofariki dunia
Na Shabani Ngarama, Karagwe
Mkuu wa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Julius Laiser amewataka watendaji wa mahakama kutenda haki kwa wananchi ili kupunguza kero na mlundikano wa kesi mahakamani
Amesema hayo Februari 3, 2025 wakati akihutubia katika kilele cha wiki ya sheria katika viwanja vya mahakama ya wilaya ya Karagwe mjini Kayanga na kusisitiza umuhimu wa kutoa haki kwa makundi mbalimbali ikiwemo kundi la wajane wanaodhulumiwa mali zao baada ya wenza wao kufariki dunia

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Karagwe Flora Haule amesema kuwa maadhimisho hayo yalitanguliwa na shughuli za utoaji elimu kwa umma kwa kushirikiana na wadau wa mahakama ambao walifundisha mada zinazohusiana na majukumu yao katika masuala ya haki jinai

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser amewataka mawakili wa kujitegemea kutoka chama cha mawakili Tanganyika TLS kuisaidia serikali kudhibiti matapeli wanaotumia mwavuli wa uanasheria ambapo mwakilishi wa mawakili wa kujitegemea amekiri uwepo wa matapeli na kutaja orodha ya mawakili wanaotambulika wilayani Karagwe