Karagwe FM
Karagwe FM
3 February 2025, 9:05 pm

Baada ya mchakato wa uchaguzi ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA ngazi ya taifa kukamilika na Tundu Lissu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti, chama hicho kimeendelea na kazi ya kusimamia nidhamu ya wanachama mikoani na wilayani
Na Theophilida Felician, Bukoba
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA jimbo la Bukoba mjini kimetangaza msimamo wake wa kuungana na chama taifa kutowatambua viongozi wa serikali za mitaa waliochaguliwa mnamo Novemba 27, 2024.
Kupitia kwa mwenyekiti wa chama hicho jimbo hilo Chifu Karumna akiwahutubia wanachama baada ya kupata taarifa ya taathimini ya uchaguzi kwenye mkutano mkuu maalumu uliofanyika katika kata ya Kashai manispaa ya Bukoba Chifu Karumna amewatangazia kwamba kuanzia sasa hawatawatambua wala kuwapa ushirikiano viongozi hao waliochaguliwa kupitia chama cha mapinduzi CCM.
Amesema kuwa uchaguzi uligubikwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukandamizaji dhidi yao kutoka kwa vyombo dola hali iliyodhoofisha ushiriki wao katika kuwapata viongozi watokanao na CHADEMA na badala yake walishinda waliokuwa wagombea wa CCM mitaa yote ya jimbo hilo.

Hata hivyo mkutano huo imeazimia kuwavua uanachama waliokuwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti baada ya kuthibitika kufanya usaliti na kujiondoa kwenye mchakato huo hatua ya mwisho kabla ya kufanyika uchaguzi