Karagwe FM
Karagwe FM
1 February 2025, 10:41 am

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser (aliyesimama). Picha na Jovinus Ezekiel
Suala la wanafunzi wa madarasa ya awali, msingi na sekondari kutoripoti shuleni kwa wakati ni changamoto inayojirudia kila mwaka wilayani Karagwe licha ya juhudi na maarifa ya viongozi kudhibiti suala hilo
Na Jovinus Ezekiel, Karagwe.
Serikali wilayani Karagwe mkoani Kagera imewaagiza waratibu elimu kata kufuatilia wazazi na walezi ambao hawajapeleka watoto wao shuleni tangu shule zilipofunguliwa Januari 13 mwaka huu
Akitoa taarifa ya serikali katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe kilichoketi katika ukumbi wa halmashauri hiyo Angaza mjini Kayanga, mkuu wa wilaya hiyo Julius Laiser amesema kuwa bado kuna wazazi na walezi ambao hawajapeleka watoto wao shuleni na kuagiza maafisa elimu kata kufuatilia sula hilo

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashuri ya wilaya ya Karagwe bw. Wallace Mashanda ameunga mkono hoja ya ufuatiliaji kwa wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni huku akipongeza ufaulu wa wanafunzi katika shule za sekondari wilayani Karagwe katika mtihani wa upimaji kidato cha pili na ule wa kidato cha nne mwaka 2024.
