Karagwe FM
Karagwe FM
29 January 2025, 10:39 pm

Serikali ya mkoa wa Kagera imeahidi kuongeza juhudi za kudhibiti magonjwa ya hatari ukiwemo ugonjwa wa Marburg uliojitokeza kwa mara ya pili ndani ya kipindi kifupi tangu uripotiwe kwa mara ya kwanza mwaka 2023 na kudhibitiwa
Na Jovinus Ezekiel, Bukoba
Serikali mkoani Kagera imeahidi kuendeleza juhudi za kupambana na ugonjwa wa Marburg ulioripotiwa wilayani Biharamulo hivi karibuni.
Akizungumuza katika mafunzo ya siku moja iliyowakutanisha waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari mkoani Kagera Januari 28. 2025 kwa lengo la kuelimishwa namna ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa huo, mkuu wa mkoa wa Kagera Hajath Fatma Mwasa amesema kuwa waandishi wa habari wanayo nafasi kubwa ya kutumia vyombo vyao vya habari kutoa elimu kwa wananchi

Ameongeza kuwa mkoa wa Kagera utaendelea kuweka juhudi za kupambana na ugonjwa huo kwa kutumia wataalam wake wa idara ya afya huku akiwasisitiza wandishi wa habari kuisaidia jamii katika kupata taarifa sahihi za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu na kudhibiti upotoshaji
Kwa upande wake afisa afya wa mkoa wa Kagera Yassin Mwinori amesema kuwa kwa sasa mkoa wa Kagera umeweka vituo maalum vya kuwahifadhi wananchi watakaogundulika na ugonjwa huo hasa katika maeneo ya wilaya za mpakani.
