Karagwe FM

Kidato cha nne Katoro sekondari watakiwa kutimiza ndoto

5 December 2024, 12:31 pm

Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM mkoa wa Kagera bw. Faris Buruhani. Picha na mpiga picha wetu

Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM mkoa wa Kagera bw. Faris Buruhan ameendelea kutoa nasaha kwa vijana hasa walioko katika shule za sekondari mara hii akiwaasa kusoma kwa malengo na kutimiza ndoto zao

Na Mwandishi wetu, Bukoba

Jumla ya wanafunzi 134 wavulana 72 na wasichana 62 wamehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya kutwa Katoro wilayani Bukoba na kutakiwa kusimamia ndoto zao, ili kukabiliana na changamoto za maisha.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kagera bw. Faris Buruhani Desemba 03, 2024 wakati akishiriki mahafali ya 14 shuleni hapo na kuwasihi vijana kukabiliana na changamoto na vikwazo vitakavyowakabili mtaani ili kukidhi kiu ya wazazi wao wanaowategemea na taifa kwa ujumla.

Aidha, amewasisitiza kuhakikisha wanasimamia ndoto zao na wala wasiogope kujaribu na kujitolea kwa kuwa elimu ya darasani ni msingi wa kuanza safari na kujua kufanikisha lakini safari ya maisha inahitaji kujituma ujasiri na ushirikiano.

Sauti ya Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kagera bw. Faris Buruhani

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo amesema shule ya sekondari ya kutwa Katoro ina mpango wa kuendelea kuboresha taaluma shuleni kwa kuwa ndio lengo kuu la shule ambayo imefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaomaliza na wanaojiunga na kidato cha kwanza.