Karagwe FM

Waislamu Karagwe wasoma dua kwa ajili ya uchaguzi

16 November 2024, 10:52 am

Sheikh wa wilaya ya Karagwe Alhaji Nassib Abdul (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa BAKWATA (W) Karagwe. Picha na Ospicia Didace

Baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kupitia msikiti wa Kihanga wamekubali ombi la Jumuiya ya vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM wilaya ya Karagwe na kufanya dua maalum kuombea taifa na uchaguzi wa serikali za mitaa na dua hiyo kuongozwa na Sheikh wa wilaya ya Karagwe Alhaji Sheikh Nasib Abdul

Na Ospicia Didace;Karagwe ,Kagera.

Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Taifa kutoka mkoa wa Kagera, Karim Amri, amewaomba viongozi wa dini kuliombea taifa na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Karim alitoa wito huo Novemba 15. 2024 katika msikiti wa Kihanga wilayani Karagwe mkoani Kagera baada ya dua maalumu iliyosomwa baada ya swala ya Ijumaa msikitini hapo kwa ajili ya kuombea taifa na viongozi na kusisitiza juu ya umuhimu wa viongozi wa dini kutumia muda wao kuimarisha amani na kuwaunganisha wanasiasa.

Dua hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Karagwe na kuongozwa na Sheikh wa wilaya ya Karagwe Alhaji Sheikh Nassib Abdul ambaye amewataka waislamu kushirikiana na serikali kukemea ukatili na mauaji

Sauti ya sheikh wa wilaya ya Karagwe Alhaji Sheikh Nassib Abdul
Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Taifa kutoka mkoa wa Kagera, Karim Amri. Kulia ni mwenyekiti wa UVCCM (W) Karagwe bw. Alexius Sylvester. Picha na Ospicia Didace

Baada ya swala na dua hiyo maalum, Karim Amri aliwashukuru waislamu kwa jitihada zao za kuliombea taifa na kuwaomba watu wenye imani zote kuomba dua wakati wote huku akiwapongeza viongozi wa dini kwa kuendelea kuwaombea viongozi wa serikali na kudumisha mshikamano miongoni mwa wanasiasa.

Sauti ya Karim Amri
Baadhi ya waumini walioshiriki dua maalum ya kuliombea taifa Kihanga, Karagwe. Picha na Ospicia Didace