Karagwe FM

Missenyi DC kuanza na milioni 95 kujenga soko la ndizi na maonyesho

5 November 2024, 5:59 pm

Wajumbe wa kamati ya fedha utawala na mipango wakiwa katika eneo la uwekezaji. Picha na Respicius John

Halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera imeendelea kutumia fursa ya uwepo wa nchi jirani ya Uganda kuibua fusa za kiuchumi kwa kubuni miradi mipya ya maendeleo itakayochochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na halmashauri hiyo

Na Respicius John

Halmashauri ya wilaya ya Missenyi imetenga shilingi milioni 95 kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa kituo cha uwekezaji chenye uwanja wa maonyesho, soko la ndizi la kisasa pamoja na stendi katika kijiji Rukurungo kata ya Bugandika

Akiongea na wandishi wa habari hivi karibuni baada ya kamati ya fedha utawala na mipango ya halmashauri ya wilaya ya Missenyi kutembelea na kujiridhisha na ukubwa wa eneo hilo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Projestus Tegamaisho amesema kuwa zimetengwa shilingi milioni 95 za kuanza ujenzi wa kituo cha uwekezaji katika eneo hilo na kuahidi kuwa baraza la madiwani linatarajia kutenga bajeti kubwa zaidi

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi bw. Projestus Tegamaisho

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Missenyi bw. Nshekanabo Nshambya amesema kuwa wao kama wawakilishi wa wananchi wamelenga kutengeneza fursa za kukuza pato la wananchi huku mhandisi wa ujenzi wa halmashauri ya Missenyi bw. Godson Ngaleo akitaja kazi zitakazoanza kwa bajeti iliyopo

Sauti ya makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Missenyi Nshekanabo Nshambya na mhandisi wa ujenzi bw. Godson Ngaleo