Karagwe FM

Wenye ulemavu wajipanga kushinda uchaguzi Kagera

13 October 2024, 5:24 pm

Katibu wa chama cha watu wasioona Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Novat Joseph Mwijage 

Wasioona ni muhimu wajiamini katika kila jambo wanalofanya kwa kuwa wana haki sawa na watu wengine wote hivyo wanapaswa kupewa ushirikiano katika jamii.

Na: Theophilida Felician -Kagera

Kuelekea chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2025 nchini vyama vya siasa vimeaswa kutokuwabagua  na kuwanyima fursa ya kuwapa dhamana ya kushiriki kugombea nyadhifa mbalimbali watu wenye ulemavu kama ilivyozoeleka.

Hayo yamebainishwa naye Katibu wa chama cha watu  wasioona TLB Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Novat Joseph Mwijage   wakati akizungumza na Redio Karagwe katika  Manispaa hiyo ambapo amesema vipindi  vya chaguzi zilizo kwisha pita asilimia kubwa watu wenye ulemavu walipojitokeza   kugombea nafasi za uongozi kwa vyama  walikwama kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya utashi mdogo wa vyama vya siasa wa kutowathamini na kuwatambua ili kuwapa nafasi za kugombea.

Sauti ya Katibu wa chama cha watu wasioona Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Novat Joseph Mwijage

Aidha amesisitiza kuwa licha ya serikali kuitoa miongozo ya kuwatambua na kuwathamini watu wenye ulemavu bado miongozo hiyo haitekelezwi kikamilifu.

Ametolea mfano wa sababu  nyingine   ambayo huwa kikwazo kwa kundi hilo  hususani kwa watu wasioona ni ile ya  usumbufu wanaokumbana nao kwa mawakala wakati wakiweka  sahihi kwenye fomu zikiwemo  fomu za chaguzi  mawakala huwataka kusaini kwa maandishi  badala ya kidole ili hali wakiwa  hawaoni.

Sauti ya katibu wa chama cha watu wasioona Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Novat Joseph Mwijage

Kiongozi huyo ambaye amegombea mara kadhaa changuzi za ndani kupitia CCM  ikiwemo nafasi mwenyekiti wa mtaa na udiwani bila mafanikio amesisitiza kuwa katu hajakata tamaa ataendelea kuthubutu zaidi.

Sauti ya katibu wa chama cha watu  wasioona Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Novat Joseph Mwijage