Kardinali Rugambwa, Dr. Bagonza wafunguka
13 October 2024, 4:18 pm
Ushirikiano wa viongozi wa dini nchini ni muhimu kuendelezwa kwa ajili ya kuchochea upendo kwa waumini na kuleta maendeleo ya kiroho na kiuchumi.
Na: Devid Geofrey – Karagwe
Muadhama Protase Kardinali Rugambwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, ametembelea Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ( K.K.K.T) kuimba na kusali na baadhi ya watumishi wa dayosisi hiyo wakiongozwa na Askofu wa Dayosisi hiyo Dr. Benson Kalikawe Bagonza.
Askofu Benson Bagonza kupitia hotuba yake, ameelezea mchango wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania katika makuzi ya Muadhama Kardinali Rugambwa.
Kwa upande wake Muadhama Protase Kardinali Rugambwa ,Pamoja na shukrani kwa uhusiano uliopo kati yake na Dayosisi ya Karagwe ya KKKT amekumbushia historia wakati akiishi katika maeneo ya Lukajange enzi zake akiwa shule ya Msingi.