Vijana wajasiriamali Mutukula wajengewa jengo la biashara
28 August 2024, 8:29 pm
Vijana wajasiriamali katika kata ya Mutukula wilayani Missenyi mkoani Kagera wamenufaika na fedha za mapato ya ndani kupitia halmashauri kwa kujengewa jengo maalum la kibiashara kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi
Na Respicius John
Kamati ya fedha utawala na mipango ya halmashauri ya wilaya ya Missenyi imeridhishwa na ujenzi wa jengo la vijana wajasiriamali Mutukula linalojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 55.7 za mapato ya ndani.
Mhandisi wa ujenzi wilayani Missenyi Winston Wilbard amesema kuwa jengo hilo litakamilika kabla ya ujio wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu wilayani humo (mwishoni mwa mwezi Septemba) na kwamba ujenzi wake unazingatia viwango. Pia Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi wakili Saraphina Rwegasira amesema kuwa jengo hilo limejengwa na serikali kwa ajili ya mafunzo kwa vijana katika nyanja mbalimbali
Baada ya kamati kutembelea na kukagu ajengo hilo makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Willy Mutayoba akasema kuwa wameridhika na utekelezaji wa mradi na kukiri kuona thamani ya fedha ambapo pia vijana watakaonufaika na mradi wameleza jinsi watakavyonufaika