Karagwe FM

Missenyi DC yaungana na CBIDO kuzuia ulemavu kupitia ‘Pamoja Program’

29 July 2024, 2:38 pm

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi wakili Sarafina Rwegasir. Picha na Respicius John

Shirika la CBIDO lililokuwa likihudumia watu wenye ulemavu wilayani Karagwe limepanua huduma zake hadi wilaya nne ambazo ni Karagwe, Kyerwa, Missenyi na Ngara mkoani Kagera kupitia mradi mpya uliopewa jina la ”Pamoja Program” utakaodumu kwa miaka 10 kwa wilaya hizo.

Na Respicius John

Shirika lisilo la kiserikali la Community Based Inclusive Development Organization CBIDO limetambulisha mradi wa pamoja utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka 10 ili kusaidia kuzuia ulemavu na kutoa huduma za utengamao kwa watu wenye ulemavu wilayani Missenyi

Meneja wa miradi ya shirika la CBIDO Donatus Kaihura. Picha na Respicius John

Katika kikao cha pamoja kilichofanyika mjini Bunazi wilayani Missenyi mkoani Kagera kikihusisha viongozi na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi meneja wa miradi ya CBIDO Donatus Kaihura ameutambulisha mradi wa Pamoja na kusema kuwa mradi huu unalenga kuzuia ulemavu na kutoa huduma za utengamao kwa watu wenye ulemavu

Sauti ya meneja wa miradi ya CBIDO Donatus Kaihura
Makamu mwenyekiti wa CBIDO mchungaji wa kanisa la Anglikana Parish ya Kayanga Odas Buchendole. Picha na Respicius John

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa shirika la CBIDO mchungaji Odas Bunchendole wa kanisa la Angilkana Parish ya Kayanga ameiomba halmashauri ya wilaya ya Missenyi kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa mradi

Sauti ya makamu mwenyekiti wa shirika la CBIDO mchungaji Odas Bunchendole wa kanisa la Angilkana Parish ya Kayanga
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Dkt Daniel Chochole.Picha na Respicius John
Sauti ya mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii Beatrice Sanga, Mganga mkuu wa wilaya ya Missenyi Dkt Daniel Chochole na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi wakili Sarafina Rwegasira
Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii wilayani humo Beatrice Sanga