Karagwe FM

EWURA CCC Kagera yapokea malalamiko 287, wananchi 9168 wafikiwa

23 July 2024, 6:14 pm

Afisa msaidizi huduma kwa wateja na utawala wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji EWURA CCC mkoa wa Kagera bi Anadorice Komba. Picha na Theophilida Felician

Kutokana na changamoto zinazowakumba watumiaji wa huduma za nishati na maji nchini, Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma hizo limekuwa na desturi ya kuwafikia na kuwashauri juu ya kutoa malalamiko yao pale wanapotendewa kinyume na matarajio

Na Theophilida Felician.

Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za maji na nishati EWURA CCC mkoa wa Kagera limebainisha kuwa katika juhudi zake za kutoa elimu kwa wananchi limewafikia wananchi 9168 kwa mwaka wa fedha 2023/ 2024.

Hayo yamesemwa na Afisa msaidizi huduma kwa wateja na utawala wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji EWURA CCC mkoa wa Kagera bi Anadorice Komba Julai 23, 2024 wakati akiongea na chombo hiki katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo katika Manispaa ya Bukoba.

Afisa huyo ameeleza kwamba njia zilizowezesha kuwafikia wananchi hao ni pamoja na kutoa elimu kwenye mikutano ya wananchi inayoandaliwa na viongozi wa serikali za mitaa, kutembelea shule, vyuo vya kati, kutoa elimu kwenye shughuli za wadau wanapokuwa wamewashirikisha, kutoa elimu kupitia klabu kadhaa zilizoanzishwa na baraza hilo na wengine kufika moja kwa moja ofisini hapo ikiwa ni sambamba na kupiga simu.

Sauti ya afisa msaidizi huduma kwa wateja na utawala wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji EWURA CCC mkoa wa Kagera bi Anadorice Komba.

Aidha amefafanua kuwa wanapowafikia wananchi zaidi ni kuwa kuwakumbusha namna ya kutambua haki na wajibu wao katika matumizi ya huduma hizo.

Amewasisitiza wananchi kutokaa kimya pale wanapoona kuna tatizo kwenye huduma, hivyo wasisite kutoa taarifa kwa watoa huduma au katika taasisi hiyo ambayo itashughulikia taarifa hiyo kwa ukaribu ili kutatuliwa.

Sauti ya afisa msaidizi huduma kwa wateja na utawala wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji EWURA CCC mkoa wa Kagera bi Anadorice Komba