Karagwe FM
Miche milioni 3 ya kahawa kugawiwa bure Karagwe
13 July 2024, 9:47 am
Uchumi wa Karagwe unaendelea kukua kutokana na hamasa ya serikali kwa wananchi juu ya kuongeza nguvu ya upandaji wa miche bora ya kahawa na kuitunza.
Na Shabani Ngarama
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe mkoani Kagera bw. Wallace Mashanda amewataka wananchi kuandaa mashimo kwa ajili ya kupanda miche ya kahawa ifikapo Oktoba, 2024 baada ya serikali kukamilisha utaratibu wa kugawa miche milioni 3 bure msimu huu.
Alisema hayo hivi karibuni baada ya kukagua kitalu kilichopo katika kijiji cha Kakulaijo kata ya Kibondo chenye miche ipatayo milioni moja kwa uratibu wa shirika la Karagwe Rural Poverty Alleviation (KARUPOA) na kuwapongeza viongozi wa shirika hilo kwa kusimamia vizuri kitalu hicho