Karagwe FM

Mradi wa maji wa miji 28 kunufaisha wananchi 164,000 Karagwe

28 June 2024, 7:51 pm

Changamoto ya upungufu wa huduma ya maji kwa wakazi wa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera inatarajiwa kupungua kwa kiasi kikubwa ifikapo Desemba 2025 baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa miji 28 maarufu kama Rwakajunju.

Na Ospicia Didace

Mradi wa maji wa miji 28 wilayani Karagwe mkoani Kagera maarufu kama mradi wa RWAKAJUNJU unaotarajia kuwanufaisha zaidi yawananchi 164,000 katika kata 12 wilayani Karagwe umefikia asilimia 20 ya utekelezaji na hadi kukamilila kwake utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 64.

Ni takribani maasaa matano yaliyotumiwa na wajumbe wa kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi CCM wilayani Karagwe ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo kukagua mradi huo wa maji almaarufu mradi wa Rwakajunju ambapo mwenyekiti wa halmadhauri ya wilaya ya Karagwe Wallace Mashanda amekiri kuwa fedha kwa ajili ya mradi huo zilishapatikana na utekelezaji unaendelea

Sauti ya mwenyekiti wa halmadhauri ya wilaya ya Karagwe Wallace Mashanda
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM wakiwa pamoja na wasimamizi wa mradi wa maji Rwakajunju. Picha na Ospicia Dodace

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa mwenyekiti wa kamati meneja wa kanda BUWASA bi Magret Nyange amesema  tayari zimefanyika shughuli mbalimbali ikiwemo utambuzi na ulazaji wa mabomba katika laini kuu,usanifu wa ujenzi wa tenki la maji pamoja na uchimbaji na umwagaji wa zege la awali kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa tenki.

Sauti ya meneja wa kanda BUWASA bi Magret Nyange
Baadhi ya mafundi wakiendelea na utandazaji wa bomba kubwa za maji. Picha na Ospicia

Mwenyekiti wa kamati ya siasa na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Karagwe bw. Paschal Rwamugata  amesema mradi huo ujengwe kwa viwango na kuwaagiza wajumbe wa kamati kuwaeleza viongozi na wananchi wa wilaya ya Karagwe juu ya maendeleo ya mradi huo.

Sauti ya mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Karagwe bw. Paschal Rwamugata na baadhi ya vijana wanaofanya kazi ya kibarua kwenye mradi

Kwa upande wake katibu wa CCM Wilaya ya Karagwe bw. Anatory Nshange akiwa kwenye chanzo yaani ziwa Rwakajunju amepongeza kazi zinazoendelea kufanyika na kusema kuwa kila mmoja anapaswa kuwa balozi ili kuondoa dhana ya kuwa mradi wa Rwakanjunju ni hadithi ya kusadikika.

Sauti ya katibu wa CCM Wilaya ya Karagwe bw. Anatory Nshange

Mradi wa maji wa Rwakajunju unaotekelezwa na mkandarasi Afcons Jv Vijeta Infrastructure Ltd unaotarajia kukamilika ifikapo Desemba 2025 kwa mujibu wa mkataba wa kandarasi utazihudumia kata 12 za wilaya ya Karagwe na kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa maji ikiwa ni baada ya serikali kupokea Dola za Marekani milioni 500 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni moja za mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya India kupitia Benki ya Exim India kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji katika miji 28