Karagwe FM

CCM Karagwe yaridhishwa na utekelezaji wa miradi ya barabara

26 June 2024, 9:58 pm

Kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Karagwe baada ya kukagua miradi ya barabara na kuridhishwa na utekelezaji wake. Picha na Ospicia Didace

Chama cha mapinduzi CCM kama chama kilichoshika dola baada ya kupata ushindi kupitia uchaguzi mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano kinalo jukumu la kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kila wilaya na maeneo yote ya nchi kuona ubora wa miradi na thamani ya fedha

Na Ospicia Didace

Kamati ya siasa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera imekagua na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya barabara zinazosimamiwa na  wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA zenye thamani ya zaidi ya shilingi billion tatu.

Moja ya barabara zilizokaguliwa na kamati ya siasa ya wilaya ya Karagwe. Picha na Ospicia Didace

Baada ya ukaguzi wa barabara hizo mwenyekiti wa kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Karagwe bw. Paschal Rwamugata ameeleza kuridhishwa na utekelezwaji wa ujenzi wa barabara hizo na kumuelekeza meneja wa TARURA wilayani Karagwe kuhakikisha utengenezaji wa barabara unasimamiwa vizuri na kuzingatia uwekaji wa karavati ili thamani ya pesa inaendana na utekelezaji wa miradi

Sauti ya mwenyekiti wa kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Karagwe bw. Paschal Rwamugata
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM wakiwa na katibu tawala wilaya ya Karagwe Rasul Shandala (mwenye shati ya drafti bila kofia upande wa kulia) Picha na Ospicia Didace

Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Karagwe Rasul Shandala ameahidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na kamati ya siasa na kuwahimiza watumiaji wa barabara kuitumia kwa matumizi sahihi ,kwani serikali inaimarisha miundombinu kwa manufaa yao na sio kwa matumizi ya usafirishaji wa biashara ya magendo

Sauti ya katibu tawala wilaya ya Karagwe Rasul Shandala
Meneja wa TARURA wilaya ya Karagwe Mhandisi Malimi Kalimbula. Picha na Ospicia Didace

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa barabara hizo meneja TARURA, Mhandisi Malimi Kalimbula ametaja mambo yatayofanyika kuwa ni pamoja na ujenzi wa makaravati na ujenzi wa mitaro kwa kiwango cha mawe

Kwa upande wao, Rehema Kibona  msimamizi mradi wa Nyarugando-Kayanga chini ya mkandarasi mzawa STARTECH COMPANY LTD na Oscar Rukanyanga chini ya mkandarasi Yunion Construction.CO.LTD ,wamesema licha ya changamoto wanazokumbana nazo  watakamilisha miradi hiyo kwa wakati kulingana na makubaliano ya mkataba.

Sauti za wakandarasi wa miradi bi Rehema Kibona na bw.Oscar Rukanyanga
Moja ya barabara zilizotembelewa na kukaguliwa na kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Karagwe. Picha na Ospicia Didace

Barabara zilizokaguliwa ni Nyarugando -Kayanga km5 itakayogharimu shilingi milion 611.5 chini ya mkandarasi mzawa M/S STARTECH COMPANY LTD, Barabara ya Nyakahanga-Masheli Kibaoni Km 3 inayojengwa kwa kiwango cha lami  kwa gharama ya shilingi billion 1.5 inayotekelezwa na mkandarasi DRK pamoja na barabara ya  Bweranyage-Kafunjo km 20 itakayogharimu shilingi  milion  904.105 na kutekelezwa na mkandarasi Yunion Construction.CO.LTD .