DC Maiga aahidi kudhibiti uchomaji moto Missenyi
15 June 2024, 6:23 pm
Na Respicius John
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi kanali mstaafu Hamisi Mayamba Maiga amezindua kampeni ya kudhibiti vitendo vya uchomaji moto mazingira huku mwenyekiti wa halmashauri ya Missenyi Projestus Tegamaisho akiomba vyombo vya dola kutoa adhabu kali kwa wachoma moto.
Akizindua kampeni hiyo inayotekelezwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) wilaya ya Missenyi inayolenga kudhibiti vitendo cha moto wilayani humo kanali mstaafu Maiga ameahidi kuunda kikosi kazi kwa ajili ya kubaini na kuchukua hatua wote wanaojihusisha na vitendo hivyo
Awali wakati akifungua mafunzo kwa wajumbe wa kamati ya maliasili kutoka katika ukanda wa tarafa ya ukanda wa Kiziba mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Projestus Tegamaisho ameiomba serikali kuchukua hatua dhidi ya watu watakaobainika wakijihusisha na uchomaji moto misitu
Kwa mujibu wa taarifa ya meneja wa TFS wilaya ya Missenyi Mrisho Juma Athumani tatizo la uchomaji moto misitu ni kubwa wilayani Missenyi ambapo baadhi ya wananchi walipewa mafunzo ya kudhibiti hali hiyo wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa umma