214 watunukiwa vyeti vya udereva kutoka VETA Kagera
11 June 2024, 1:05 pm
Wimbi la madereva wa vyombo vya moto waisiokuwa na mafunzo wala leseni limeendelea kupungua nchini siku hadi siku kutokana na mikakati ya serikali na wadau wanaoratibu mafunzo ya jumla yanayotolewa kwa ufadhili wa taasisi au mashirika na kuwawezesha washiriki kupata mafunzo na leseni kwa muda mfupi na gharama nafuu.
Na Ospicia Diace
Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser amefunga mafunzo ya madereva wa magari na pikipiki pamoja na kuwatunuku vyeti wahitimu 214 wa walioshiriki mafunzo hayo huku akiwataka kuzingatia yote waliyofundishwa ili kupunguza ajali za barabarani.
Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyoendeshwa na VETA Kagera kwa ufadhili wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Karagwe Laiser aliwataka madereva hao kuutumia ujuzi walioupata katika kuepusha ajali zisizo za lazima.
Akiongea wakati wa kufungwa kwa mafunzo hayo Mkurugenzi wa VETA Kagera Winston Kabantega na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Karagwe bw. Paschal Rwamugata wamewaomba maderevaa hao kuwa mabalozi wazuri kwa madereva wengine.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilayani Karagwe mkaguzi wa polisi Deusdedit Muguha amesema kuwa kuna sababu tatu za ajali ambapo ajali zinazotokana na mtu mwenyewe inaongoza kwa aslimia 76.