Watoto kukosa chakula shuleni ni chanzo cha lishe duni Missenyi
11 June 2024, 12:14 pm
Kumekuwa na changamoto kubwa ya lishe kwa watoto mkoani Kagera ambapo baadhi ya shule zilibuni mkakati wa kuwezesha wanafunzi kupata lishe shuleni. Hata hivyo baadhi ya wazazi hawaoni umuhimu wa kuchangia lishe ya watoto wao wawapo shuleni.
Na Respicius John
Uelewa mdogo kwa watoa huduma za afya ngazi ya jamii pamoja na utelekezaji wa watoto na familia vimetajwa kuwa kikwazo cha utoaji huduma za lishe wilayani Missenyi mkoani Kagera. Katika taarifa ya lishe kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/2024 iliyosomwa na afisa lishe bi Faustina Godwin kwa wajumbe wa kamati ya lishe wilaya ya Missenyi imebainisha baadhi ya changamoto huku akitaja baadhi ya shughuli zilizofanyika chini ya ofisi yake
Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii wilaya ya Missenyi Evance Mvungi alitumia kikao hicho kuwataka akina mama wilayani humo kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya wakati wa ujauzito kupata elimu ya lishe kwa wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano
Naye afisa elimu taaluma wilaya ya Missenyi mwalimu Maijo amesema kuwa idara ya elimu msingi inaendelea na juhudi za kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe shuleni kwa wingi