Karagwe FM

Mkoa wa Kagera wafikia 93% ya lengo la upandaji miti

8 June 2024, 7:16 pm

Mkuu wa wilaya ya Missenyi kanali mstaafu Hamis Maiga akimwagilia mche wa mti alioupanda hivi karibu akiadhimisha siku ya mazingira. Picha na Respicius John

Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera ni moja kati ya maeneo yenye changamoto ya watu wanaoharibu mazingira nyakati za kiangazi kwa kuchoma moto mapori na misitu licha ya wilaya hii kuzungukwa na maeneo mengi ya uhifadhi chini ya wakala wa huduma za misitu (TFS) kama vile msitu wa Minziro wenye vivutio vingi vya utalii

Na Respicius John

Wananchi mkoani Kagera wametakiwa kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa wingi sambamba na kudhibiti vitendo vya uchomaji moto hovyo ili kuepusha athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi. Wito huo ulitolewa na mkuu wa mkoa wa Kagera katika hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Missenyi kanali mstaafu Hamis Maiga aliyemwakilisha katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Kagera kata ya Kyaka na kuwasisitiza wananchi kuendelea kutunza mazingira na kupanda miti zaidi ambapo hata hivyo mwenyekiti wa halmashauri ya Missenyi Projestus Tegamaisho aliomba serikali kutoa tamko kuzuia uchomaji moto.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Projestus Tegamaisho (mwenye kisemeo). Picha na Respicius John
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Missenyi kanali mstaafu Hamis Maiga na mwenyekiti wa halmashauri ya Missenyi Projestus Tegamaisho
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Missenyi Alhaji Saidi Seluu akiwaasa wanafunzi kutunza mazingira. Picha na Respicius John

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Missenyi Alhaji Saidi Seluu aliwasihi wanafunzi kushiriki shughuli za utunzaji mazingira na kuwahimiza wazazi na walezi kupanda miti huku kaimu mkuu wa kitengo cha maliasili na mazingira Aloyce Mchonde akieleza shughuli zinazofanywa na halmashauri ya wilaya kudhiti uharibifu wa mazingira

Sauti ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Missenyi Alhaji Saidi Seluu pamoja na kaimu mkuu wa kitengo cha maliasili na mazingira Aloyce Mchonde
Baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Kagera wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya mazingira mkoa wa Kagera