DC Maiga awapa matumaini ya ajira walimu wa shule binafsi Missenyi
31 May 2024, 6:38 pm
Kumekuwa na kasumba kwamba walimu wanaofundisha katika shule binafsi hawawezi kupata ajira serikalini hali inayowafanya kukata tamaa na kubaki wakibembeleza ajira zao hata kama mazingira ya kazi ni magumu.
Na Respicius John
Mkuu wa wilaya ya Missenyi mkoani Kagera kanali mstaafu Hamis Mayamba Maiga amewataka walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani humo kuendelea kujitolea katika maeneo wanakohudumu na kuongeza ubunifu zaidi katika masomo wanayofundisha ili kuwashawishi waajiri na wanafunzi kuwaamini.
Alisema hayo Mei 29, 2024 wakati wa ziara yake ya siku moja katika shule ya awali na msingi ya kiingereza Bunazi Green Acres iliyoko kata ya Kassambya alikokagua hali ya miundombinu ya shule hiyo na kuwasisitiza walimu kuongeza juhudi na bidii ili viwatangaze walimu hao katika soko la ajira hata serikalini.
Meneja wa shule ya awali na msingi ya kiingereza Bunazi green acres bi Namala Tibanga amemshukuru mkuu wa wilaya ya Missenyi kwa ushirikiano na shule hiyo na kumhakikishia kuwa uhusiano huo unafanywa pia na watumishi walioko chini ya ofisi ya mkuu wa wilaya wakisimamia sekta ya elimu na kwamba wanajivunia kufanya kazi wilayani Missenyi