Karagwe FM

Malumbano ya viongozi yachelewesha ujenzi wa sekondari ya kata

11 May 2024, 5:51 pm

Katibu wa CCM wilaya ya Karagwe Anathory Nshange akitoa kadi za chama kwa mmoja wa wanachama waliotoka vyama vya upinzani na kujiunga na CCM. Picha na Ospicia Didace.

Mara nyingi viongozi kushindwa kuelewana hali inayosababisha kuchelewesha miradi ya maendeleo ya wananchi hasa upande wa uamuzi wa wapi mradi ujengwe jambo linalowaumiza wananchi wa chini wanaosubiri kunufaika na mradi husika.

Na Ospicia Didace.

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Anathory Nshange amewataka viongozi wa chama na serikali katika kata ya Ndama kuacha mivutano na kufanya vikao vya makubaliano na maamuzi juu ya eneo la kujengwa shule ya sekondari katani humo.

Alisema hayo hivi karibuni akiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika tawi la Kagutu kata ya Ndama kwa lengo la kuwapokea wanachama wapya zaidi ya 30 waliojiunga na chama hicho.

Ni wanachama waliojiunga na chama cha mapinduzi CCM wakila kiapo cha ahadi za mwanachama. Picha na Ospicia Didace.
Sauti ya katibu wa ccm wilaya ya Karagwe Anathory Nshange.

Nshange amewapongza wanachama hao kwa kujiunga na ccm akisema kuwa chama kinaendelea na utekelezaji wa ilani hivyo wamefanya maamzi sahii na kueleza kuwa kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme pamoja na maji serikali iko mbioni kupeleka huduma hiyo katika maeneo yao.

Katibu wa ccm wilaya ya Karagwe Anathory Nshange (aliyeunganisha viganja vya mikono) akifurahia jambo na wanachama wenzake. Picha na Ospicia Didace

Pamoja na hayo ametumia mkutano huo kuwakanya viongozi wa kata ya Ndama kuacha mivutano ya kuamua ni wapi shule ya sekondari ijengwe kati ya kijiji cha Nyabwegira na kijiji cha Kagutu akisema kuwa kutokana na mivutano hiyo wanaoendelea kuumia ni watoto wao.

Sauti ya katibu wa CCM wilaya ya Karagwe Anathory Nshange

Nao baadhi ya wanachama waliojiunga na chama cha mapindizi kutoka vyama vya upinzani wamesema kuwa wanaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwani kwenye eneo lao hawakuwa na zahanati lakini sasa huduma ya afya inapatikana karibu pamoja na kukata tamaa ya kukosa ushindi kila uchaguzi.

Sauti za baadhi ya wanachama waliojiunga na chama cha mapinduzi.

Hata hivyo Katibu wa CCM wilaya ya Karagwe Anathory Nshange amewakumbusha wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la kujiandikisha kwenye dafratari la kudumu la wapiga kura ili kuboresha taarifa zao ili kupata nafasi ya kushiriki kwenye chaguzi zijazo.