CCM Kagera: Rweikiza ametekeleza ilani kwa kishindo
21 April 2024, 5:21 pm
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Nazir Karamagi. Picha na Abdullatif Yunus
Chama chochote cha siasa huandaa ilani kama dira ya kutekeleza vipaumbele vya mahitaji ya wapiga kura pindi kinaposhika dola baada ya uchaguzi mkuu wa viongozi.Chama cha mapinduzi CCM kimepokea na kuridhia taarifa ya utekelezaji wa ilani yao jimbo la Bukoba vijijini kwa kipindi cha miaka mitatu .
Na Muhammad Mkurumbona
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Kagera Alhaji Nazir Karamagi amewashukuru wanachama kwa ushirikiano wao kwa viongozi wa CCM katika kazi ya kuwaletea maendeleo. Amesema kuwa maendeleo yanayoletwa na viongozi wa CCM si mafanikio yao bali ni mafanikio ya chama kwa sababu hata ikitokea viongozi wakafanya uzembe chama ndicho hubeba dhamana.
Amesema hayo Aprili 20, 2024 baada ya mbunge wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Samson Rweikiza kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha miaka mitatu kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Bukoba.
Amempongeza Dk. Rweikiza kwa mafanikio makubwa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuwaasa viongozi wa chama kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya chaguzi zijazo.
Sauti ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Alhaji Nazir Karamagi
Mbunge wa Bukoba vijijini Dk. Rweikiza. Picha na Abdullatif Yunus
Kwa upande wake mbunge wa Bukoba vijijini Dk. Rweikiza ameishukuru serikali na wadau wa maendeleo kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo jimboni kwake kwa kipindi cha miaka mitatu akijivunia ukamilifu wa miradi ya barabara na maji
Sauti ya mbunge wa Bukoba vijijini Dk. Rweikiza
Karim Amri, MNEC mkoa wa Kagera. Picha na Abdullatif Yunus
Naye mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka Mkoa wa Kagera Karim Amri amewashukuru madiwani kwa ushirikiano mzuri kwa mbunge wao na kuwaasa kuacha siasa za ubaguzi ili waendelee kupata miradi mikubwa ya maendeleo
Sauti ya Karim Amri, MNEC mkoa wa Kagera