Miss Mkoa kukabidhiwa Ndinga ya kisasa.
27 May 2021, 8:26 am
Mchakato wa Kumpata Mrembo atakayewakilisha Mkoa wa Kagera katika Shindano la Miss Tanzania 2021, umeanza kushika Kasi katika Mkoa wa Kagera, Baada ya Kamati ya Maandalizi kwa kushirikiana na Waandaaji Kutambulisha Rasmi zawadi ya Mshindi wa Taji hilo.
Akitambulisha zawadi hiyo mratibu wa Shindano la Miss Kagera 2021 Regina Zachwa kutoka Zachwa Investment, amesema Mwaka huu wao Kama waandaaji waliopewa dhamana hiyo, kwa kushirikiana na Serengeti Breweries Ltd pamoja na Wadau wengine wameamua kuandaa zawadi ya Gari Mpya, aina ya Rectus yenye Thamani ya Shilingi Milioni 18 ambayo atapewa Mshindi wa Kwanza katika Shindano hilo.
“..Mara hii Miss Kagera itakuwa Kivingine na kubwa zaidi, ukizingatia Ukubwa wa zawadi ya Mshindi, lakini pia wapo Baadhi ya waheshimiwa wakiwemo Wabunge ambao wameamua kussuport Jambo Hili, hivyo tunategemea pia ushindani utakuwa Mkubwa Sana…” Amesema Regina.
Zawadi hiyo ya Gari imezinduliwa Rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe Deodatus Kinawiro katika Viwanja vya Makao Makuu ya Redio Kasibante FM inayomilikiwa na Zachwa Investment, ambaye kwa Upande wake amesema Shindano hilo litautangaza Mkoa wa Kagera katika nyanja tofauti zikiwemo za kiuchumi na kiutamaduni, na kuwataka wasichana kujitokeza kushiriki katika mchakato huo.
Pamoja na Mambo mengine Kamati hiyo ya Maandalizi ya Shindano la Miss Kagera, imeweka wazi ratiba ya Shindano hilo kwa Wilaya za Mkoa Kagera ambapo Mwezi Mei Tarehe 28 na 29 Shindano litaanzia Biharamulo na Ngara, Mwezi ujao itakuwa zamu ya Muleba na Missenyi, Mwezi wa Saba zamu ya Karagwe na Kyerwa na Kisha kilele cha Shindano ni Agosti 08, 2021 ndani ya Bukoba Manispaa.