Timu ya Nyaishozi SC kutua Bungeni wiki hii
27 April 2021, 12:02 pm
Na Shabani Ngarama, Karagwe FM
Timu ya Nyaishozi kutoka wilaya ya Karagwe iliyowakilisha mkoa wa Kagera kwa kupanda daraja la pili katika michuano ya fainali ya ligi za mikoa iliyofanyika mkoani Lindi imepata fursa ya kupumzika Dodoma wakati ikitokea mkoani Lindi ikiwa imeibuka mshindi wa tatu katika mashindano hayo.
Credit: Eliud Rwechungura
Jumanne Asubuhi April 27. 2021 Nyaishozi SC ikiwa safarini kurejea Karagwe ilifika makao makuu ya nchi, Jijini Dodoma na kupokelewa na Waziri mwenye dhamana ya Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo Innocent Bashungwa
Kutokana na heshima waliyoipatia wilaya ya Karagwe anakotokea waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Karagwe, Waziri huyo ameiomba timu nzima kupumzima kwa siku mbili na hatimaye April 28 watapata heshima ya kutembelea na kutambulishwa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Timu ya Nyaishozi SC wamekuwa maarufu siku za nyuma kutokana na ligi ya Mbunge Innocent Bashungwa iliyoendeshwa kwa miaka miwili mfululizo na kuwaibua vijana wengi wa wilaya ya Karagwe wanaopenda mpira wa miguu