Zenj FM
Zenj FM
14/03/2026, 18:13

Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kamesheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame, yamelenga kuwajengea uwezo masheha ili kufahamu wajibu wao.
Na Hakika Mwinyi.
Masheha wametakiwa kuyafanyia kazi Mafunzo waliyopatiwa pamoja nakufahamu wajibu wao pindi yanapotokea maafa katika Shehia zao.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu Kamesheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Makame Khatib Makame wakati akifungua mafunzo ya elimu ya kukabiliana kwa Masheha wa Wilaya ya Kati hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Manispaa Kati Dunga.
Amesema Masheha wanatakiwa kufahamu wajibu wao na nafasi zao pindi yanapotokezea maafa katika Shehia hizo kwakuanzisha kamati za maafa za shehia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Kati Dk Mwanaisha Ali said amesema lengo la kuwaandalia masheha mafunzo hayo ni kuona wanafuata taratibu zote pindi yanapotokezea maafa katika Shehia zao kabla yakuripoti sehemu husika.
Nao Masheha waliyopatiwa mafunzo hayo Wamesema bado baadhi ya wananchi hawana uwelewa pindi wanakumbwa na maafa katika jamii zao.
Jumla ya Masheha 42 wa wilaya ya Kati wamepatiwa mafunzo hayo ya siku moja ili kufahamu wajibu wao na nafasi zao katika kukabiliana na maafa.