Zenj FM

Manispaa Kati yatoa onyo kali kwa wamiliki wa viwanja na magofu

16 February 2026, 2:24 pm

Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa Kati Said Hassan Shaaban akizungumza na Wananchi wa maeneo ya Jumbi na Tunguu IPA eneo la kuta la ZSSF Wilaya ya Kati Unguja.

Na Hakika Mwinyi.

Wananchi wametakiwa kusafisha maeneo yao  yaliyo wazunguka pamoja na kuhakikisha Viwanja na Magofu vinakuwa safi kwa usalama wao na Jamii kwa ujumla.

Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa Kati Said Hassan Shaaban ameyasema hayo wakati wa shughuli ya Usafi wa Mazingira shughuli iliyofanyika maeneo ya Jumbi Uwandani na Tunguu IPA eneo la kuta la ZSSF Wilaya ya Kati Unguja.

Amesema ni jambo la muhimu wamiliki wa Viwanja na Magofu ambayo yamekuwa yakisababisha uwepo wa mwitu na vichaka nivyema wachukue jitihada ya kusafisha maeneo yao, na iwapo watashindwa Serikali itachukua hatua zinazo faa kuhakikisha maeneo hayo yanakuwa safi na salama kwa maslahi ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.

Sauti ya Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa Kati Said Hassan Shaaban

Nae Diwani wa Wadi hiyo ya Tunguu Hadhar Abdallah Hadhar kwaniaba ya Madiwani wenzake amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kila mara inapotokea fursa ya Usafi wa pamoja na kuendelea kufanya Usafi Kila kila siku kwani Usafi ni jukumu la Kila mwananchi.

Sauti ya Diwani wa Wadi hiyo ya Tunguu Hadhar Abdallah Hadhar.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Kati Daktari Mwanaisha Ali Said amesema suala la Usafi ni jukumu la Kila mmoja Baraza la Manispaa husaidia kwa kutoa mashirikiano ya pamoja ili kufanikisha Usafi huo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Kati Daktari Mwanaisha Ali Said.

Nao Wananchi wa Tunguu na Jumbi wamesema wameridhishwa na hatua iliyochukuliwa na Baraza la Manispaa Kati kwa kufanya Usafi kwa pamoja pia wameiomba  Manispaa hiyo kuwatengea sehemu maalumu za kuekea taka ili kuhakikisha taka hazitupwi ovyo na kuchafua Mazingira.

sauti za Wananchi wa Tunguu na Jumbi.

Usafi huo umewajumuisha Madiwani wa Baraza la Manispaa Kati, Watendaji wa Manispa hiyo na Wananchi wa maeneo ya Jumbi Uwandani na Tunguu IPA eneo la kuta la ZSSF Wilaya ya Kati Unguja.