Zenj FM

Mahakama Kuu ya Zanzibar yatupilia mbali maombi ya zuio la kuteketeza nyaraka za uchaguzi

13 February 2026, 5:01 pm

Mahakama Kuu Zanzibar

Mary Julius.

Mahakama Kuu ya Zanzibar imekubaliana na pingamizi lililowekwa na Tume ya uchaguzi Zanzibar pamoja na mwanasheria  mkuu wa serikali na kuyatupilia mbali maombi ya kuweka zuio la kuteketeza nyaraka za uchaguzi yaliyowasilishwa na wagombea wa ACT Wazalendo.

Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Salma Hassan, ambaye amesema mahakama imejiridhisha kuwa wakili aliyesaini hati za viapo za waombaji hao  hayo hakuwa leseni ya ukamishina wa viapo wakati wa kuwasilisha maombi hayo, jambo linalokwenda kinyume na matakwa ya kisheria.

Akizungumza nje ya Mahakama, Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo, Omar Said Shaaban amekiri kuwa wakili aliyewaapisha waombaji hakuwa amehuisisha leseni yake ukamishina wa viapo  wakati akitekeleza jukumu hilo.

Sauti ya Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo, Omar Said Shaaban.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kurugenzi ya Huduma za Sheria, ZEC Maulid Ame Mohammed, amesema uamuzi huo unaonesha umuhimu wa kuzingatia taratibu na matakwa ya kisheria katika uwasilishaji wa maombi mahakamani.

Sauti ya Mkuu wa Kurugenzi ya Huduma za Sheria, ZEC Maulid Ame Mohammed.