Zenj FM

Wilaya ya Kati yajipanga upya baada ya tathmini ya matokeo 2025

11 February 2026, 9:33 pm

Afisa Elimu Wilaya ya Kati, Somoe Said Mussa, akitoa ufafanuzi wa tathmini matokeo ya mitihani ya kidato cha pili na cha nne kwa mwaka 2025, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa ofisi ya Elimu Kidimni Wilaya ya Kati Unguja.

Na Hakika Mwinyi Mwaka.

Walimu wametakiwa kufanya tathmini ya masomo yao mara kwa mara ili kuhakikisha wanafunzi wanapata uelewa wa kutosha wakiwa madarasani, hatua itakayochangia kuongeza ufaulu wao kitaaluma.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Elimu Wilaya ya Kati, Somoe Said Mussa, katika mkutano wa kutathmini matokeo ya Kidato cha Pili na Kidato cha Nne kwa mwaka 2025. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Afisi ya Elimu Kidimni, Wilaya ya Kati.

Afisa Elimu amesema walimu, wazazi pamoja na Wizara ya Elimu wanapaswa kusimamia kikamilifu majukumu yao ili kuhakikisha ufaulu unaongezeka, hususan katika skuli za Wilaya ya Kati.

Sauti ya Afisa Elimu Wilaya ya Kati, Somoe Said Mussa,

Kwa upande wake, Afisa Taaluma Sekondari, Hamdu Zuber Ameri, amesema tayari wameanza kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha matokeo, ikiwemo kuanzisha kambi za masomo mapema kwa wanafunzi wanaojiandaa na mitihani.

Sauti ya Afisa Taaluma Sekondari, Hamdu Zuber Ameri,

Akizungumza kwa niaba ya wazazi, Mwenyekiti wa Skuli ya Kibele, Iddi Ame Manzi, amesema wazazi wamekubaliana na maamuzi yaliyotolewa na Wizara ya Elimu na wako tayari kushirikiana kwa karibu ili kuona watoto wao wanafaulu kwa kiwango cha juu.

Sauti ya Mwenyekiti wa Skuli ya Kibele, Iddi Ame Manzi.

Mkutano huo wa tathmini umehusisha skuli 30 za Kidato cha Pili na Kidato cha Nne kwa mwaka 2025 kutoka Wilaya ya Kati, ukishirikisha kamati za skuli, walimu wa taaluma, wenyeviti pamoja na masheha.