Zenj FM
Zenj FM
5 January 2026, 8:18 pm

Na Berema Nassor.
Waziri wa mawasiliano Teknolojia ya habari na ubunifu Mudrik Ramadhan Soraga amesema lengo na dhamira ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuanzisha taasisi ya wakala wa ulinzi JKU ni kuhakikisha serikali inapata mapato yatokanayo na huduma za ulinzi kutoka katika sekta ya utalii uwekezaji na biashara.
Hayo ameyaeleza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ofisi ya wakala wa ulinzi Jku Mtoni amesema wakati umefika sasa kwa wakala wa ulinzi JKU kuzidisha ubunifu na kujituma zaidi ili kuweza kutoa huduma kwa serikali na taasisi binafsi kwa lengo la kupata mafanikio kwa maslahi ya taifa na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maluum za SMZ Mikidadi Mbarouk Mzee amesema lengo la mradi huo ni miongoni mwa kuboresha mazingira bora na rafiki kwa watumishi wa wakala wa ulinzi JKU.
Nae Mkuu wa Utawala wa JKU Zanzibar Kanal Haji Ali Ali ameahidi kwamba ujenzi huo utakidhi viwango na ubora unaotakiwa kwa lengo la kufanya kazi kwa bidii na weledi zaid.
Uwekaji wa jiwe la msingi la ofisi ya wakala wa Ulinzi Jku Mtoni ni miongoni mwa shamrashamra za maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi matukufu Zanzibar.