Zenj FM

Wito watolewa kuhifadhi mazingira

11 December 2025, 6:31 pm

Waandishi wa habari wadau wa utalii pamoja na viongozi wa TANAPA wakiwa katika lango kuu la kuingia katika hifadhi ya mlima wa Udzungwa.

Na Mary Julius.

Ikiwa leo dunia inaadhimisha Siku ya Milima Duniani, jamii ameihimiza kutambua wajibu wa kutunza na kuhifadhi mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Katika maadhimisho hayo, Zenji fm imezungumza na Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa, Hilary George , ambaye amebainisha umuhimu mkubwa wa milima kwa ustawi wa maisha ya binadamu.

Hilary amesema kuwa milima inabeba hazina muhimu ya kiikolojia na kiuchumi, akifafanua kuwa maji safi duniani hutokana na milima, jambo linaloifanya kuwa uti wa mgongo wa ustawi wa jamii nyingi.

Aidha, ameeleza kuwa milima ni makazi ya viumbe hai adimu, mimea na wanyama wanaopatikana sehemu chache duniani, hivyo kuifanya kuwa kitovu muhimu cha bioanuwai.

Sauti ya Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa, Hilary George.

Hata hivyo, pamoja na umuhimu huo, Hilary ameeleza kuwa milima inakabiliwa na changamoto nyingi zinazotokana na shughuli za kibinadamu.

 Ameitaja ukataji ovyo wa miti, uharibifu wa misitu, uchafuzi wa mazingira na ongezeko la shughuli za kibinadamu kama miongoni mwa vitisho vikubwa vinavyoathiri mfumo mzima wa kiikolojia wa milima.

Sauti ya Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa, Hilary George.

Kadhalika, Hilary ameiomba serikali na wadau mbalimbali kuendeleza ushirikiano katika shughuli za uhifadhi, ikiwemo kufanya tafiti na kutoa fedha zitakazowezesha kulinda maeneo ya milima kwa ufanisi zaidi.

Sauti ya Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa, Hilary George.

Kila ifikapo Desemba 11, dunia huadhimisha Siku ya Milima Duniani,.