Zenj FM
Zenj FM
10 December 2025, 9:06 pm

Na Mary Julius.
Katika harakati za kuimarisha mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Zanzibar, Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya UKIMWI Zanzibar, Khamis Haroun Hamad, ameibuka na kampeni kabambe inayolenga moja kwa moja wanafunzi wa vyuo vikuu, kundi ambalo limebainika kuwa na tabia hatarishi zinazopelekea uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi mapya .
Akizungumza katika uzinduzi wa bonanza michezo liliendana sambamba na upimaji wa la afya lililofanyika katika chuo kikuu cha Zanzibar SUZA Kampasi ya Biashara ya Chwaka, Afisa huyo amesema kuwa Mkoa wa Kusini unaendelea kuongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi, kwa upande wa Zanzibar jambo lililowasukuma kuongeza kasi ya kutoa elimu na upimaji kwa wanafunzi wa chuo na jamii ninayoizunguka vyuo vikuu.
Amefafanua kuwa mpango huo si tukio la siku moja pekee, bali ni mkakati endelevu, unaolenga kuhakikisha elimu inawafikia wanafunzi na jamii ya Zanzibar mara kwa mara.
Ameongeza kuwa Tume ya UKIMWI inashirikiana na wadau mbalimbali ili kuwasaidia wale wote watakaobainika kuwa na maambukizi, kuhakikisha wanapata tiba, ufuatiliaji na ushauri stahiki ili waendele kuishi kwa kufuata miongozo ya afya.
Kwa upande wake, Mlezi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Ahmad Rashid Ramadhani, amepongeza mpango huo akisema unakwenda sambamba na jitihada za chuo kuhakikisha afya za wanafunzi, hasa wale wapya, zinaimarishwa.
Nae Sheha wa Shehia ya Chwaka, Ali Hassan Mjombo, amekaribisha mpango huo kwa mikono miwili akieleza utayari wake kutoa ushirikiano wa aina yoyote ili elimu hiyo ifike mbali zaidi.
Nao baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wamesema hatua hiyo ni faraja katika kuona ni namna gani serikali inavyoendlea kujali afya za wananchi wako, na kusisitiza kuwa ni vyema fursa kama hizo za uchunguzi na elimu ya afya zikawa endelevu kwa maslahi ya wote.
Bonanza hili lilipambwa na michezo mbalimbali, ikiongozwa na mpira wa miguu, kukimbia kwa magunia, kukuna nazi .