Zenj FM

Waziri Sharif akabidhi idara Tatu, atoa wito wa kasi na matokeo kwa watendaji

3 December 2025, 9:51 pm

Waziri wa Kazi na Uwekezaji Zanzibar, Sharif Ali Sharif, akikabidhi idara tatu kutoka Wizara ya Kazi na uwekezaji kwenda Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji.

Na Mary Julius.

Waziri wa Kazi na Uwekezaji Zanzibar, Sharif Ali Sharif, ametoa wito kwa wafanyakazi wa Idara ya Ajira, Idara ya Maendeleo ya Ushirika, na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ZEEA kuongeza bidii na kusimamia majukumu yao kwa ufanisi ili kuhakikisha maelekezo ya Rais wa Zanzibar yanatekelezwa kwa kasi na matokeo.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya idara hizo kutoka Wizara ya Kazi na uwekezaji kwenda Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji, halfa iliyo fanyika katika ukumbi wa wizara ya kazi na uwezeshaji mwanakwelekwe .

Waziri Sharif amesema mabadiliko yaliyofanyika si ya bahati mbaya, bali ni mkakati wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na fursa za ajira.

Waziri amewataka Wafanyakazi wote  kusimamia ipasavyo majukumu yao ili kumsaidia Rais na Baraza la Mapinduzi kufanikisha malengo ya wananchi.

Aidha, Waziri Sharif amekabidhi rasmi idara tatu zenye jumla ya wafanyakazi 149, na kusisitiza kuwa vipimo vya utendaji vitafanyika kwa muda wa miezi mitatu.

Sauti ya Waziri wa Kazi na Uwekezaji Zanzibar, Sharif Ali Sharif,

Kwa upande wake, Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Shaaban Ali Othman, ameahidi kushirikiana na watendaji wote kwa kasi na matokeo, akisisitiza kuwa wizara yake itaendelea kushirikiana na Wizara ya Kazi na Uwekezaji ili kuhakikisha wananchi wananufaika ipasavyo.

Aidha Waziri shaabani amesema atahakikisha anasimamia ukamilishaji wa Sheria ya ajira ili kutoka fursa ya utekelezaji unaokwemda sambamba na Matakwa ya kisheria.

Sauti ya Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Shaaban Ali Othman.