Zenj FM
Zenj FM
1 December 2025, 7:49 pm

Na Mary Julius.
Zaidi ya wageni 150 hadi 400 wanawasili katika hifadhi ya taifa ya Mikumi kwa siku kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kikoboga kutokana na uboreshaji wa kiwanja hicho, uliofanywa na TANAPA.
Afisa Uhifadhi Mwandamizi wa Hifadhi ya taifa ya Mikumi, Hellen X. Mchaki, ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa utalii kutoka Zanzibar waliotembelea kiwanja hicho, amesema wageni wengi hufika kwa day trip, wachache hukaa kwa kulala,.
Ameeleza kuwa katika kipindi cha low season hifadhi hupokea ndege kubwa kati ya 3 hadi 7 na ndege ndogo 2 hadi 3, huku katika high season idadi ikiongezeka hadi kufikia ndege kubwa 8 hadi 15 na kuendelea pamoja na ndege ndogo 8 ,kati ya ndege hizo nyingi hutoka Zanzibar na nyingine zikitokea maeneo ya Arusha Dar es salam na kwingineko.
Nao Watalii waliotembelea hifadhi hiyo kwa njia ya anga kutoka Zanzibar wamesema wamechagua Tanzania kwa sababu ni nchi yenye amani na watu wakarimu, na wameichagua Mikumi kutokana na uwepo wa wanyama wakubwa wa aina mbalimbali.
Aidha Wameahidi kuendelea kuitangaza hifadhi hiyo ili wageni wengi zaidi wafike kushuhudia vivutio vyake.
Kwa upande wake, Rubani wa kampuni ya Jambo Aviation, Kapteni Hamamad Hassan, amesema wageni wengi huanza safari zao Zanzibar kwa shughuli za baharini na kuogelea, na baada ya kuitangaza hifadhi ya Mikumi wageni wamevutiwa kutembelea hifadhi hiyo
Kapteni Hassan ameongeza kuwa Tanzania ina vivutio vingi vinavyowavutia wageni, huku kivutio kikubwa kikiwa ni amani ya nchi.
Aidha, ameshauri TANAPA kuhakikisha ujenzi wa kiwanja cha ndege unakamilika ili kuongeza ufanisi wa mapokezi ya wageni.
Akizungumzia mchango wa filamu ya royal tour Kaptein amesema filamu hiyo imesaidia kupunguza low season na kufanya wafanye kazi kwa kipindi kirefu na hivyo kuongeza pato la taifa na jamii kwa ujumla.