Zenj FM
Zenj FM
1 December 2025, 7:20 pm

Na Mary Julius.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itahakikisha inaongeza Bajeti katika kusimamia utoaji wa huduma za afya kwa watu wanao ishi na virusi vya ukimwi ili kuimarisha upatikanaji wa huduma hizo kwa uhakika hayo yamebainishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali itahakikisha Sheria na Sera zote zinazingatiwa na zinalindwa dhidi ya ubaguzi na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya unakuwa wa haki kwa wote bila ya ubaguzi.
Amesema Zanzibar imefanikiwa kupunguza maambulizi mapya ya maradhi ya kimwi kutoka watu 362 kwa mwaka 2020 hadi kufikia watu 211 waliopata maambukizi mapya kwa mwaka 2025 jambo lililosaidi kupunguza vifo vitokanavyo na maradhi hayo kutoka vifo 230 kwa mwaka 2020 hadi vifo 115 kwa mwaka 2025.
Aidha Hemed amewasihi wananchi kutowanyanyapa na kuwabagua watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kwani kufanya hivyo ni kudhorotesha jitihada za Serikali za kumaliza maambukizi mapya ya Ukimwi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ukimwi Dkt. Ali Salim Ali amesema juhudi za kuzuia maambukizo ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto zimezidi kufanikiwa kwa kuonesha maendeleo chanya ya maambukizo yaliyo chini ya asilimia mbili ikiwa ni hatua ya kufikia lengo la kumaliza maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Aidha, katika kuhakikisha usawa wa upatikanaji wa huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi hasa wanaume ushirikiano katika jamii unazidi kuimarishwa ili kuondoa vikwazo vinavyowazuia wanaume kupata huduma muhimu za matibabu ya VVU.
Akisoma risala ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Zanzibar Sara Abdi Mwita amesema kutokana na Mashirika wafadhili kusuasua katika kutoa misaada hasa kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wanaiomba Serikali kuliangalia suala la dawa za ARV kuwekwa katika bajeti ya serikali ili huduma hio iendelee kuwa endelevu kwa wagonjwa wa Ukimwi.