Zenj FM

Zena Ahmed Said: Mwanamke aliyepanda kilele cha madaraka Zanzibar

17 October 2025, 7:00 pm

Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zena Ahmed Said.

Na Ivan Mapunda

Kila safari kubwa huanza kwa hatua moja, na hatua ya Zena Ahmed Said zimemfanya kuwa nyota halisi inayong’aa katika utumishi wa umma.

Hadithi yake ni ushuhuda wa uwezo wa uthabiti, uadilifu na ufuatiliaji usio na kikomo wa ubora, ukichochea kizazi cha wanawake kuvunja vizuizi na kufafanua upya  matumaini na Uwezekano kwa wanawake .

Eng Zena Said aliweka historia januari 2021, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo adhimu.

Safari Ya Maisha Na Elimu.

Eng  Zena Ahmed Said ni wwanamke mwenye historia ya kipekee katika uongozi wa serikali na utumishi wa umma. Kwa sasa, anahudumu kama Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, nafasi ambayo inamhusisha moja kwa moja katika usimamizi wa masuala ya kiutawala na utekelezaji wa sera za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Zena Ahmed Said amezaliwa  mkoa wa Tanga  na ameolewa na Hamidu Majallah Athumani Tangu Juni 1992 na ni mama  watoto watatu wawili wakike na moja wa kiume .

Elimu yake ya awali  alipata katika skuli ya msingi ya  Ubungo National Housing mwaka 1985.

Na Baadae alijiunga na  skuli  ya Jangwani  secondary school  alisoma  Kidato cha nne na cha sita  Kutoka mwaka 1986 Mpaka mwaka 1992 .

Aliendelea na masomo mpaka kufika degree ya kwanza ya uhandisi   Uturuki  katika chuo cha  Boğaziçi University. Mnamo mwaka 2010 alihitimu shahada ya uzamili katika usimamizi wa ununuzi wa umma kutoka chuo kikuu cha Turin nchini italia, na mwaka 2020 alichukua diploma ya uzamili katika diplomasia ya uchumi.

Uzoefu wa Uongozi

Alifanya kazi kwa muda mfupi katika sekta binafsi na COWI Consult kama msimamizi wa ujenzi kuanzia mwaka 2000 hadi 2002.

Baadae aliajiriwa katika afisi za wakala wa barabara nchini (TANROADS) katika ukanda wa Pwani ya Tanzania bara.

Alianza katika Kurugenzi ya Matengenezo ambapo alifanya kazi kama mhandisi wa matengenezo na baadaye kurugenzi ya manunuzi.

Aliuchukua likizo bila malipo na kufanya kazi na Benki ya Dunia Ofisi ya nchi ya Tanzania kama mshauri kutoka 2006 hadi 2008 ambayo ilimuweka kwenye utamaduni wa kimataifa wa kazi.

Mwaka 2016, Hayati Rais Dk John Pombe Magufuli alimteua kuwa katibu tawala wa mkoa wa Tanga, uteuzi wa kihistoria uliotambua umahiri wake na maadili yake ya kazi yasiyoyumba.

Baada ya takribani miaka minne akiwa Tanga, Zena aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, ambapo aliitumikia kwa muda wa miezi 11 kabla ya Kuteuliwa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwa Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi.

Kinacho msukuma kufanya kazi kwa bidii

Kinachonisukuma Kwanza ni mwenyezi Mungu  kwa sababu kazi ni ibada lazima ni ifanye na pili ni Yule aliyeniteua na jamii kwa ujumla ,Mimi nataka kuwa mfano bora .

“Mwanamke akifeli aonekani yeye kama individual wanaonekana wanawake wote wamefeli  ,mtu akuhumiwe yeye kama  individual  “anasema zena

Pia nataka familia yangu na watoto wangu wawe mfano mzuri.

changamoto na mafanikio.

Katika nafasi yake ya sasa, Zena Ahmed Said ameonyesha uwezo mkubwa wa kusimamia mambo kwa umakini, akihakikisha utendaji kazi bora wa taasisi za serikali.

Anajulikana kwa mtazamo wake wa kiubunifu, uwazi, na uwajibikaji, mambo ambayo yameimarisha ufanisi wa serikali na kuleta maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.

“Kila nafasi unayopewa ifanye kwa juhudi na nguvu zako zote  ili uweze kukidhi matarajio ya waliokuteuwa ,kila kazi inamisingi yake na  kazi inatakiwa ichukuliwe kama ibada utakiwi kupindisha. “Anasema Zena

Changamoto kwenye kazi huwa hazikosekani ila unatakiwa kuangalia misingi ya utendaji inataka nini na watu wanafanyaje tofauti sababu wanazofanya tofafauti .

Mtazamo Wa Kijinsia

Zena anasema, jinsia haijawahi kuwa kisingizio cha yeye kushindwa kuwajibika wala kugeuka takrima kwenye nafasi za uongozi.

Amepinga dhana potofu, na mfumo dume ambao umeishi kwa muda mrefu na kusema kuwa kwa sasa taratibu mfumo  umeanza kubadilika na kutoa fursa kwa wanawake na kuwapa chachu wanawake kufanya vizuri katika nafasi walizopewa .

“Mwanamkwe ndio mwalimu wa kanza ,Ni muhimu kuwapa fursa wanawake za elimu   stahiki hiyo ndo inajenga msingi wa mustakabali wa baadae”. Anasisitiza Zena

Maadili Uwazi na Uadilifu

Zena Ahmed Said anasifika kwa kuwa kiongozi anayejali maadili, anayejituma, na mwenye maono makubwa. Ni mfano bora wa uongozi wa kiadilifu na mwenye kushughulikia changamoto kwa njia ya busara na mbinu za kiutawala zinazozingatia maslahi ya jamii.

Mtindo wake wa kuongoza  ni  alama mahususi za uongozi mageuzi katika ulimwengu wa kisasa ulio ngumu,kwa Zena, uongozi ni zaidi ya cheo au vyeo ni kuhusu jinsi watu wanavyotendewa.

“Kila binadamu anastahili heshima awe amesoma au la. Hatupaswi kumdharau mtu yeyote kwa sababu ya nafasi yake,” Anasema Zena.

Ushawishi wa Kijamii

Mbali na majukumu yake ya kiserikali, Zena Ahmed Said amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za kijamii, hususan zinazolenga kuwainua wanawake na vijana. Amejikita katika kuhamasisha usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika uongozi na shughuli za kiuchumi.

Ndoto Ya Kuwa Mhandisi

Wakati nakua siku na role model ambaye alikua mhandisi  kwenye familia fani nilizokuwa nazijua ni  uwalimu, udaktari, nesi na afisa wa polisi.

“Sijawahi kufikiria kama nitakuja kuwa muhandisi  , ni kudra za mwenyezi Mungu tu”. Anasisitiza Zena

Pia kuingia kwake kwenye fani ya uhandisi kulichangiwa na masharti ya mkopo wa elimu kusoma masomo yanayohusiana na sayansi baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari kwa matokeo bora, Eng Zena alifanya chaguo ambalo lilikiuka matarajio ya jamii alipokuwa akiolewa. Ingawa wengi walidhani huu ungekuwa mwisho wa matarajio yake ya kitaaluma, kwa zena ulikuwa mwanzo tu.

“Haikua fani niliyokuwa nimeipanga wala kuipenda “.Anaeleza Zena

Majukumu Na Malezi Ya Watoto

Kwa Zena, uongozi sio leseni ya kuachana na maisha ya familia. Badala yake, ni wito wa kufaulu katika kila jukumu – kitaaluma na kibinafsi. Hadithi yake inapinga masimulizi ya uwongo ambayo wanawake wanapaswa kuchagua kati ya familia na kazi. Yeye ni dhibitisho kwamba wote wawili wanaweza kuishi pamoja na heshima na mafanikio, akisisitiza umuhimu wa kupanga na mshirika msaidizi.

“Mimi ni mama mwenye upendo kwa watoto wangu na mume wangu napenda sana kutumia muda wangu na familia yangu ” Anasema Zena

Ushauri Kwa Wanawake

Wanawake watende haki kwa nafasi waliyokabidhiwa.

“Wajue wazi kwamba majukumu mengine kamwe hayapaswi kuathiri majukumu yao rasmi”. Anasema Zena

Lakini, kwa wale walio katika nafasi ya kusaidia na kuwawezesha wanawake, “nasema waendelee kuwaunga mkono na kuwawezesha licha ya majukumu ya kifamilia ambayo yanaweza kujitokeza mara kwa mara”. Anasisitiza Zena