Zenj FM

Zanzibar yawekeza kwenye elimu ya watoto wa awali kufikia dira ya 2050

5 October 2025, 8:27 am

Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Masoud Omar Masoud, akizungumza katika mahafali ya tano ya Turkish Maarif Kindergarten yaliyofanyika Mombasa, Zanzibar.

Na Ivan Mapunda.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya elimu ili kuhakikisha taifa linafikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya 2050.

Akizungumza katika mahafali ya tano ya Turkish Maarif Kindergarten yaliyofanyika Mombasa, Zanzibar, Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Masoud Omar Masoud, amesema serikali imeongeza bajeti ya sekta hiyo ili kuboresha ubora wa elimu nchini.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu na kuandaa mazingira rafiki kwa mashirika binafsi yanayowekeza katika sekta hiyo, ili kuharakisha utekelezaji wa dira ya maendeleo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Masoud Omar Masoud.

Aidha, Masoud amewataka wazazi kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya watoto wao ili kuhakikisha wanafikia malengo yao kielimu.

Sauti ya Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Masoud Omar Masoud.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miradi wa SOS, Asha Salim Ali, amewasisitiza wazazi na walezi kuwalea watoto katika misingi ya maadili mema na kuwapatia elimu bora inayowaandaa kuwa viongozi wa baadaye.

Sauti ya Mkurugenzi wa Miradi wa SOS, Asha Salim Ali,

Naye Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Turkish Maarif Kindergarten, Amina Suleiman Saleh, amesema shule hiyo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 232, ambapo 70 kati yao wamehitimu mwaka huu wanaume 38 na wanawake 32, wote wakiwa na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuonyesha maadili bora.

Sauti ya Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Turkish Maarif Kindergarten, Amina Suleiman Saleh.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi, Katibu wa Kamati ya Wazazi, Subira Abdallah, amewashukuru walimu na uongozi wa shule kwa kazi nzuri ya kuwalea watoto katika misingi bora ya elimu na maadili.