Zenj FM
Zenj FM
3 September 2025, 5:00 pm

Na Is-haka Mohammed.
Wakati waumini wa dini ya Kiislamu wakitarajia kusheherekea maadhimisho ya kuzaliwa kwa Kiongozi wao wa Umma Mtume Muhamad (SW) wametakiwa kufuata mienendo na maisha aliyokuwa akiishi Mtume ikiwemo mapenzi, umoja na mshikamano kwa jamii.
Hayo yemelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Alhaji Rashid Hadid Rashid wakati akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kupokea matembelezi ya Maulid ya Uzawa wa Mtume Muhammad (S.A.W) yalionzia Bazara la Manispaa Chake Chake hadi Viwanja vya Kumumzikia Madungu yaliyokuwa na lengo la kuhamasisha amanoi na uhamasishaji wa kushiriki kwenye maulid.
Amesema Mtume Muhammad (S.A.W ) alikuwa ni muumini mkubwa wa amani, umoja na upendo kwa jamii yake, akifahamu kuwepo na kupendana kwa watu katika jamii ni kujenga misingi imara ya kuishi katika amani na utulivu.
Kwa upande wake Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais, Katiba na Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Halima Ali Khamis amesema kuwa amewataka waislamu kuendelea kuishi kwa maono na miongozo ya Mtume Muhammad S.A.W.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mratibu Ofisi ya Mufti Mkuu Pemba Shekh Said Ahmad Mohamed amesema Ofisi hiyo kwa kushirikiana na Kamati ya Maulid wamedhamiria kufanya shughuli mbali mbali katika harakati za kuadhimisha maulid kuanzia mwaka huu.
Matembelezi hayo yaliyoanzia Baraza la Manispaa Chake Chake hadi katika Bustani ya Mwanamashungi ni sehemu ya ramsha rabsha za kuadhimisha uzawa wa Mtume Muhammad SAW, ambapo kilele kitafanyika Kesho katika kiwanja cha Polisi Madungu ambapo Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdulla Akitarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.