Zenj FM

Afisa elimu awataka wanafunzi kuwa makini vyuo vikuu

24 August 2025, 12:21 am

Afisa Elimu Mkoa wa Mjini Magharibi, Mohamed Abdalla Mohamed, akitoa zawadi kwa mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza katika hafla ya kuwapongeza iliyoandaliwa na skuli ya Kiponda.

Na Mary Julius.

Afisa Elimu Mkoa wa Mjini Magharibi, Mohamed Abdalla Mohamed, amewataka vijana waliohitimu kidato cha sita Skuli ya Kiponda kuendeleza juhudi zao za kujisomea ili kufanikisha ndoto zao na kuliletea taifa maendeleo.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wanafunzi hao wa mwaka 2025, iliyo fanyika katika skuli ya sekondari ya Dimbani Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja Mohamed amesema utaratibu wa kuwapongeza wanafunzi ni muhimu kwa kuwa unawatia moyo na kuongeza ari ya kujituma zaidi.

Aidha, amewataka wanafunzi watakaojiunga na vyuo vikuu kuwa makini, kuepuka vishawishi vinavyoweza kuharibu mustakabali wao, na kusoma kwa bidii ili kufanikisha malengo yao.

Sauti ya Afisa Elimu Mkoa wa Mjini Magharibi, Mohamed Abdalla Mohamed.

Akizungumzia uchaguzi mkuu afisa elimu amewataka kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo.

Sauti ya Afisa Elimu Mkoa wa Mjini Magharibi, Mohamed Abdalla Mohamed.

Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Kiponda, Ayoub Yussuf Khamis, amesema matokeo ya mwaka 2025 yanaonyesha mafanikio makubwa ambapo wanafunzi 37 walipata daraja la kwanza, 38 daraja la pili na 8 daraja la tatu.

Sauti ya Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Kiponda, Ayoub Yussuf Khamis.

Naye Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kiponda, Miza Kai, Khamisi amesema matokeo mazuri ya shule hiyo yametokana na mazingira bora yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi, kupitia Wizara ya Elimu.

Sauti ya Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kiponda, Miza Kai, Khamis.

Nao wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao wamesema siri ya mafanikio yao ilikuwa ni kumweka Mungu mbele, nidhamu, kujitolea muda na hata fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya kujisomea, pamoja na mshirikiano kati yao.

Wakizungumzia changamoto walizokutana nazo, wanafunzi hao wamesema uhaba wa madarasa ulikuwa kikwazo kikubwa kwani kusoma kwa shifting (vya zamu) kulipunguza ari ya kujifunza.

Sauti ya Wanafunzi.