Zenj FM
Zenj FM
16 August 2025, 4:39 pm

Na Mwandishi wetu
Kamishina mstaafu wa Tume ya kurejebisha Katiba Tanzania Nassor Khamis Mohamed amesema aliyekuwa Balozi wa Cuba Humphire Polepole anapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kufunguliwa mashitaka kwa Manufaa ya Taifa na kulinda misingi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Khamis amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari huko Kisahuni Mkoa wa mjini Magharibi Unguja kuhusu madai ya Polepole kupiga uteuzi wa Rais DK Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dk Hussen Ali Mwinyi kuwa wagombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi mwaka huu.
Nassor amesema vitendo vinavyofanywa na Polepole vinatia aibu viongozi wa Tume ya kurekebisha Katiba Tanzania wakiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba.
Akuzungumzia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar amesema umeleta manufaa makubwa kwa pande zote mbili na kutaka misingi ya muungano kuendelea kuimarishwa kwa manufaa Taifa.
Aidha amesema baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu muhimu marekebisho ya Katiba ya Tanzania yakafanyika ili kuwa na Katiba bora zaidi.
Aliyekuwa Balozi wa Cuba Humphire Polepole ameibua mjadala mkubwa kwa wanasiasa na wanaharakati baada ya kudai Kuna kasoro katika kuwapata wagombea wa Urais wa Muungano na Zanzibar huku baadhi ya wanachama wakitaka afukuzwe uanachama kwa kwenda kinyume na miiko na maadili ya Chama.