Zenj FM

Dakika 3 tu kituoni, agizo la RC kwa madereva wa daladala

15 August 2025, 4:44 pm

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa akizungumza wakati wa ziara aliyofanya ya kutembelea baadhi ya vituo vipya vya daladala ambavyo vimeanza rasmi kutumika.

Na Mary Julius.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa, amewataka madereva wa daladala kuzingatia matumizi sahihi ya vituo vipya vya kushushia na kupakia abiria, kwa kuhakikisha hawazidi dakika tatu katika kila kituo, ili kuepuka msongamano wa magari na kurahisisha harakati za usafiri jijini.
Ametoa wito huo leo wakati wa ziara aliyofanya kutembelea baadhi ya vituo vipya vya daladala ambavyo vimeanza rasmi kutumika.
Amesema amesema serikali imeamua kuweka vituo hivyo ili kurahisisha huduma kwa wananchi na kuboresha mfumo wa usafiri wa umma.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi kuzingatia usafi wa mji kwa kutokutupa taka ovyo, ili kuhakikisha mji unakuwa safi na wenye mvuto kwa wakazi na wageni.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wameushukuru uongozi wa mkoa kwa kuruhusu vituo hivyo vipya, wakieleza kuwa awali walikuwa wakipata shida kubwa katika kufikia maeneo ya usafiri.

Sauti ya wananchi.

Nao madereva wa daladala wamepongeza hatua hiyo ya serikali, wakisema imekuwa ni msaada mkubwa kwao na kwa abiria, na wameahidi kuzingatia masharti ya matumizi ya vituo hivyo.