Zenj FM

Wilaya ya Kusini kusafisha majaa yasiyo rasmi

7 August 2025, 4:23 pm

Msaidizi Afisa mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Biubwa Hassan Haji, akizungumza wakati wa zoezi la usafi katika maeneo ya Mbuyuni Shehia ya Jambiani Kibigija.

Msaidizi Afisa mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Biubwa Hassan Haji, amesema Halmashauri inaandaa utaratibu wa kuanzisha vikundi maalum kwa kila Shehia vitakavyohusika na uchukuaji taka za majumbani.

NA Khamis Abdi Juma

Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja imewaomba wananchi wa Wilaya ya Kusini kuunga mkono kampeni ya usafi wa mazingira ndani ya Wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa zoezi la usafi katika maeneo ya Mbuyuni Shehia ya Jambiani Kibigija ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kuondosha majaa yasiyo rasmi katika Wilaya ya Kusini Msaidizi Afisa mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Biubwa Hassan Haji amesema kuwa lengo la zoezi hilo ni kuhakikisha Halmashauri inaondosha majaa yote yasiyo rasmi ili kuleta haiba nzuri ya Wilaya hiyo.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuunga mkono jitihada hizo ili kuondosha tatizo la utupaji taka kiholela ndani ya Wilaya hiyo.

Sauti ya Msaidizi Afisa mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Biubwa Hassan Haji.

Kwa upande wake Sheha wa Shehia ya Jambiani Kibigija Sinatama Makame Haji ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Kusini kwa kuamua kushirikiana nao kufanya usafi katika enoe hilo.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kutodharau wanapopata taarifa ya kuwepo mazoezi kama hayo.

Sauti ya Sheha wa Shehia ya Jambiani Kibigija Sinatama Makame Haji.

Nao wananchi wa maeneo hayo wametoa wito kwa wananchi wenzao kuacha tabia ya kutupa taka ovyo ili kujiepusha na maradhara yanayoweza kutitokeza.

Sauti ya Wananchi.