Zenj FM

CHAMATA yaelimisha vijana kuhusu ajira kupitia miradi ya serikali

4 August 2025, 2:43 pm

Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan, akifungua kongamano la kuibua miradi ya maendeleo ambayo imefanywa na Rais wa Zanzibar Dk Hussen Ali Mwinyi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan, kwa niamba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana.

Na Mary Julius.

CHAMA cha Mama Tanzania (CHAMATA) kimesema kuna fursa nyigi za kunufaika na ajira kwa Vina kupitia miradi ya Maeneleo ikiwemo soko la sekta ya utalii, miudo mbini Kilimo na mawasiliano lakini bado hazijatumika ipasavyo Tanzania bara na Visiwani Zanzibar.

Hayo yameleezwa na Katibu mkuu wa Chama hicho Perter Christopher Ngwele, katika kongamano la kuibua miradi ya maendeleo ambayo imefanywa na Rais wa Zanzibar Dk Hussen Ali Mwinyi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan.

Sauti ya Katibu Mkuu wa Chama CHAMATA Perter Christopher Ngwele,

Ngwele amesema wameamua kutoa elimu kwa vijana mikoa yote juu ya miradi ya maendeleo iliyofanyika na fursa za ajira kama watatumia vizuri kupitia miradi hiyo.

Sauti ya Katibu Mkuu wa Chama CHAMATA Perter Christopher Ngwele,

Akifungua kongamano hilo kwa niamba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan amewataka vijana kujiepusha na mambo yanayo sababusha umasiki ikiwemo uvuvu na matumizi ya sitarehe.

Sauti ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan.
Mkuu wa Wilaya ya kusini Unguja Othiman Ali.

Akifunga kongamano hilo Mkuu wa Wilaya ya kusini Unguja Othiman Ali amewataka vijana kuendelea kudumisha amani na umoja wa kitaifa katika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya kusini Unguja Othiman Ali.

Kongamano la vijana Kizimkazi limefanyika katika ukumbi wa skull ya kizimkazi na kuhudhuliwa na Viongozi wa Chama cha Mama Tanzania (CHAMATA) kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.

Mada tatu ziliwasilishwa katika kongamano hili ikiwemo miradi ya maendeleo iliyotekelezwa, kijana na uchumi na kijana na nishati safi.