Zenj FM
Zenj FM
30 July 2025, 12:20 pm

Katibu wa Chama Cha Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi Tanzania, Timoth Funto,aAkizungumza mara baada ya ziara katika viwanda vya kutengeneza viatu vya Idara Maalum za SMZ vilivyopo Mtoni, Wilaya ya Magharibi 'A'Ili kuhimiza matumizi ya rasilimali ya bidhaa za ngozi, Katibu wa Chama Cha Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi Tanzania, Timoth Funto, ametangaza kuanzishwa kwa mradi wa kutengeneza viatu vya ngozi milioni 10 vitakavyosambazwa katika skuli mbalimbali nchini.
Na Mary Julius.
Katibu wa Chama Cha Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi Tanzania, Timoth Funto, amesema zaidi ya viatu milioni 54 vya ngozi huagizwa kutoka nje ya nchi kila mwaka kwa gharama kubwa, licha ya Tanzania kuwa na rasilimali kubwa ya ngozi inayoweza kuzalisha viatu hivyo ndani ya nchi.
Akizungumza mara baada ya ziara katika viwanda vya kutengeneza viatu vya Idara Maalum za SMZ vilivyopo Mtoni, Wilaya ya Magharibi 'A', Funto amesema bado kuna changamoto katika matumizi ya ngozi kama rasilimali ya ndani kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zenye thamani kama viatu.
Amesema iwapo ngozi ya ng’ombe na wanyama wengine itatumika ipasavyo, basi vijana wengi watanufaika kwa kupata ajira kutokana na uanzishwaji wa viwanda vya kutengeneza viatu nchini.
Aidha, amesema viatu vya ngozi kutoka Tanzania vinathaminiwa sana nje ya nchi, lakini bado havijapata nafasi stahiki katika soko la ndani.
Katibu wa Chama Cha Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi Tanzania, Timoth Funto.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa viwanda vya Idara Maalum za SMZ, SSP Ramadhan Khamis Ibrahim, amesema wamejipanga kushirikiana na wadau mbalimbali kuanzisha chama cha ngozi Zanzibar ili kuhakikisha rasilimali hiyo inatumika ipasavyo na kuleta tija kwa viwanda na biashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa viwanda vya Idara Maalum za SMZ, SSP Ramadhan Khamis Ibrahim.Kwa upande wake, Afisa kutoka Taasisi ya Viwango Zanzibar, Mhammed Juma Khamis, amesema taasisi yao iko tayari kushirikiana na wadau kuhakikisha bidhaa zitokanazo na ngozi zinazingatia viwango bora ili kuvutia masoko ya ndani na nje ya nchi.
Afisa kutoka Taasisi ya Viwango Zanzibar, Mhammed Juma Khamis.