Zenj FM
Zenj FM
29 July 2025, 7:22 pm

Tamasha la vijana Kizimkazi linatarajiwa kuwakutanisha vijana wasiopunguwa 450 pamoja na watalam wa masuala ya uchumi, biashara, fedha na nishati kupitia mabaraza ya vijana Zanzibar.
Na Mary Julius.
Chama cha Mama Tanzania (CHAMATA) kimesema utafiti waliofanya wamegundua kuna miradi mingi ya maendeleo inatekelezwa na serikali zote mbili ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar lakini bado wananchi hawaifahamu na kushindwa kuzitumia fursa zilizopo kupitia miradi hiyo.
Katibu wa chama hicho Peter Christophar Ngwele ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la vijana Kizimkazi ambalo linatarajiwa kufanyika Agost 3 mwaka huu Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema kutokana na hali hiyo chama hicho kimeamua kuitisha kongamano la vijana kizimkazi Kusini Unguja ili watalamu waweze kutoa mafunzo wa vijana yatakayowasiadia kufahamu miradi iliyotekelezwa na fursa zilizopo miradi hiyo.
Aidha ameyataja maeneo yaliyopiga hatua kubwa imaendeleo ikiwemo afya,miundombinu,kilimo na mawasiliano na huduma za usafiri ikiwemo teni ya mwendo kasi.
Amesema Rais Samia ameonyesha kuwapa kipaombele kikubwa vijana kwa sababu ndio nguvu kazi ya taifa na ameahidi vijana wengi watanufaika na nafasi za katika vyombo vya maamuzi ikiwemo ubunge,uwakilishi na nafasi zingine za uteuzi.

Mkuu wa wilaya ya Kusini Unguja, Othman Ali Maulid. Naye Mkuu wa wilaya ya Kusini Unguja, Othman Ali Maulid amesema tamasha hilo ni fursa nzuri kwa vijana kujifunza mbinu mbalimbali ziitakazoweza kuwasaidia kujiajiri ikiwemo kupitia sekta ya utalii.
Mkuu wa wilaya ya Kusini Unguja, Othman Ali MaulidTamasha la vijana Kizimkazi linatarajiwa kuwakutanisha vijana wasiopunguwa 450 pamoja na watalamu wa masuala ya uchumi,biashara,fedha na nishati kupitia mabaraza ya vijana Zanzibar.