Zenj FM
Zenj FM
16 July 2025, 3:12 pm

Wamiliki wa gari za abiria wasiopungua kumi na tano 15 na madereva wa ruti za Wilaya ya Kati wamepatiwa elimu ya usafi katika gari zao.
Na Mwandishi wetu.
Wamiliki wa gari za abiria na madereva wametakiwa kuzingatia suala la usafi katika gari zao kwa kueka madastibini ili kuepusha abiria kutupa taka ovyo barabarani.
Mkurugenzi wa Baraza la Mji Kati Dkt Mwanaisha Ali Said ameyasema hayo wakati wakitoa elimu ya usafi kwa madereva na wamiliki wa gari za abiria hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Mji Kati Dunga Wilaya ya Kati.
Aidha Amesema kunatabia ya baadhi ya abira wakiwa kwenye gari hutupa taka nje ya gari hali inayopelekea uchafuzi wa mazingira katika jamii na mji hupoteza haiba yake.
Kwa upande wake Malik Bakari ambae ni Katibu Mtandao wa Jumuiya za usafirishaji abiria na mizigo Zanzibar amewaomba Baraza la Mji Kati kutoa elimu kwa wamiliki na madereva mara kwa mara ili kuhakikisha lengo linafikiwa.
Naye Katibu Mtandao wa jumuiya ya usafirishaji abiria na mizigo Wilaya ya Kati Issa Daudi Suleiman amesema maagizo waliyopewa na Baraza la Mji Kati watayafanyia kazi kuhakikisha mji unabaki katika haiba nzuri.
Akizungumza kwa niaba ya madereva na wamiliki wa gari za abiria Hussein Mussa Foum ameeleza kuwa watakuwa wadau wa kuhamasisha jamii kuimarisha usafi si tu katika gari na hata katika mazingira yao yaliyowazunguka.
Wamiliki wa gari za abiria wasiopungua kumi na tano 15 na madereva wa ruti za Wilaya ya Kati wamepatiwa elimu hiyo kuimarisha usafi katika gari zao.