Zenj FM

Jamii yatahadharishwa meno ya watoto yako hatarini

4 July 2025, 4:46 pm

Daktari wa meno kutoka hospitali ya Remedy clinik Kkhamis Zubeir Khamis akizungumza katika zoezi la kuwafanyia uchunguzi na kutoa elimu juu ya maradhi ya kinywa kwa wanafunzi wa skuli ya baby Care semta ya Jumbi.

Jamii imetakiwa kuona umuhimu wa kuwafanyia uchunguzi wa afya watoto ili kuweza kugundua tatizo na kupatiwa matibabu mapema.

Na Mary Julius.

Jamii nchini imeshauriwa kujiwekea utaratibu wa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya ili kufanyiwa uchunguzi wa maradhi mbali mbali ikiwemo ya kinywa na meno.

Akizungumza katika zoezi la kuwafanyia uchunguzi na kutoa elimu juu ya maradhi ya kinywa kwa wanafunzi wa skuli ya baby Care semta ya Jumbi daktari dhamana kutoka hospitali ya Remedy clinik Dokta Abubakar Kombo Omar amesema hatua hiyo itasaidia kupungua kwa wimbi kubwa la watoto wanao athiriwa na maradhi hayo.

Amesema kumekua na ongezeko kubwa la watu wengi hasa watoto kuharibika meno kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ukosefu wa elimu ya usafi wa kinywa, kula vyakula vyenye sukari.

Sauti ya Daktari dhamana kutoka hospitali ya Remedy clinik Dokta Abubakar Kombo Omar.

Kwa upande wake daktari wa meno hospitali hiyo Kkhamis Zubeir Khamis ambae ameshiriki katika zoezi la uchunguzi amesema kati ya watoto 48 waliofanyiwa uchunguzi wengi wao wamebainika tayari meno yao yameshaharibika.

Sauti ya Daktari wa meno Kkhamis Zubeir Khamis.

Nae Msaidizi Mwalim Mkuu skuli ya Semta Zahra Juma Kheri amezisifu juhudi za hopitali hiyo kwa uamuzi wa kuwafanyia uchunguzi wanafunzi skulini hapo na amewataka wazazi ambao watoto wao wamegundulikana na athari ya maradhi hayo kuwapeleka hospitali kupatiwa matibabu kwa lengo la kuimarisha afya za vinywa.

Sauti ya Msaidizi Mwalim Mkuu skuli ya Semta Zahra Juma Kheri.